Wednesday, April 6, 2016

Na Mwanahamisi Issa
Aliewahi kuwa mbunge wa mbagala Dkt. mohamed Dau, leo ametangaza rasmi kuachana na masuala ya siasa kufuatia haliya sintofahamu iliyojitokeza mapema hivi karibuni.

akizungumza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake mtaa wa mabatini, Dkt Dau , amesema kuwa, yeye na familia yake wameridhia hatua hiyo ya kuachana kwake na masuala ya kisiasa kufuatia vitisho mbalimbali anavyovipata kutoka kwa watu asio wafahamu.